Bugando yaboresha matibabu kwa wenye vichwa maji na mgongo wazi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wazazi na walezi wa watoto wenye matatizo ya vichwa maji na mgongo wazi
wamehimizwa kuwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa
Bugando iliyopo jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu badala ya kuwaficha
nyumbani wakidhani matatizo hayo yanatokana na imani za kishirikina.
Hayo yalielezwa jana Julai 22, 2019 na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji
katika Hospitali ya Bugando, Dkt. Fabian Massaga baada ya Hospitali hiyo kupokea
ugeni kutoka Shirika la “Child-Help International” ambalo limekuwa likifadhili
uboreshaji wa matibabu ya vichwa maji na mgongo wazi hospitalini hapo.
Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake ana tatizo la kichwa kikubwa
aliushukru uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kutoa bure huduma ya upasuaji
kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huku akishauri Hospitali hiyo
kupunguza gharama za dawa na vipimo ikiwemo “CT-Scan” kwani bado ni changamoto
kwao.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: