LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya MISA Tanzania yatoa mafunzo kwa viongozi wa vyombo vya habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tawi la Tanzania, imeandaa warsha kwa viongozi (wahariri na mameneja) wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini ili kuwajengea uwezo kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Warsha hiyo ya siku tano imeanza leo jumatatu Julai 22, 2019 jijini Mwanza lengo kuu likiwa ni kuimarisha utendaji kazi wa viongozi hao katika kutoa habari linganifu pamoja na kupata mbinu za jinsi ya kujilinda wakiwa katika mazingira hatarishi ya kazi.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amesema miongoni mwa mada zitakazowasilishwa kwenye warsha hiyo ni pamoja na umuhimu wa kuripoti habari linganifu hususani kipindi cha uchaguzi, nafasi ya mwanamke katika vyombo vya habari na chaguzi mbalimbali.

Gasirigwa amezitaja mada nyingine kuwa ni jukumu la vyombo vya habari katika kukuza demokrasia, uandishi unaozingatia maadili, usalama wa waandishi wa habari mtandaoni pamoja na mazingira hatarishi ya waandishi wa habari.

Washiriki wamesema warsha hiyo ni muhimu kwao katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi mdogo mwaka huu 2019 pamoja na uchaguzi mkuu hapo mwakani 2020 na kwamba elimu watakayoipata watahakikisha inawafikia waandishi wa habari wengine katika vyombo vyao vya habari.

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania imeshirikiana na taasisi ya IREX ya nchini Marekani pamoja na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kufanikisha warsha hiyo inayotarajiwa kufikia tamati ijumaa Julai 26, 2019.
 Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akitoa neno la ufunguzi kwenye warsha hiyo inayofanyika Adden Pallace Hotel jijini Mwanza.
 Sarah Bushman kutoka taasisi ya IREX akitoa salamu zake kwenye warsha hiyo.
 Ben Ellis kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania akisisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia weledi katika utendaji wao wa kazi.
 Mshiriki Fredy Herbert kutoka Bomba FM ya jijini Mbeya akiwasilisha maoni ya washiriki wenzake kupitia makundi.
Mshiriki Juma Khamis kutoka gazeti la Zanzibar Leo akichangia mada kwenye warsha hiyo.
 Jacquiline Lawrence ambaye ni Meneja wa Highlands FM ya jijini Mbeya akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Mshiriki Joas Kaijage kutoka Kagera Community Radio akichangia mada kwenye warsha hiyo.
 Mhariri kutoka Clouds Media Group, Joyce Shebe akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
 Washiriki wamekiri kwamba warsha hii ni muhimu kwao wakati ambao Tanzania inaelekea kwenye chaguzi.
Scolastica Mazula kutoka EFM Radi akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Mshiriki Alex Mchomvu kutoka SAUT akisisitiza jambo kwenye warsha hiyo.
 Washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
 Washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
 Washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
 Wawakilishi kutoka taasisi ya IREX na Ubalozi wa Marekani wakifuatilia warsha hiyo.
 Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania ikiwemo magazeti, redi la luninga.
 Washiriki wakiwa kwenye majadiliano.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakijadiliana kwa njia ya makundi.

No comments:

Powered by Blogger.