LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mzozo wasababisha watu wanne kupoteza maisha wilayani Ukerewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Watu wanne wamepoteza maisha katika Kisiwa cha Siza kilichopo Wilaya Ukerewe mkoani Mwanza, kufuatia mzozo baina ya wananchi na maafisa wa kikosi cha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema tukio hilo limetokea leo Julai 22, 2019 ambapo wananchi wanne wamepigwa risasi na kusababisha watatu miongoni mwao kufariki papo hapo huku mmoja akikimbizwa katika Hospitali ya Nansio kwa matibabu.

Mongella amebainisha kwamba mtu wa nne aliyefariki ni kiongozi wa kikosi hicho chenye jukumu la kudhibiti na kutokomeza uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi katika Ziwa Victoria ambaye ameshambuliwa na wananchi huku pia askari mmoja akijeruhiwa ambapo naye amekimbizwa katika Hospitali ya Nansio.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.