Header Ads

Wazee wa koo Tarime wabadilishia gia angani “wanajamii wabaki njia panda”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Baadhi ya wazee wa koo kutoka kabila la Wakurya Wilaya Tarime mkoani Mara wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto awamu ya pili 2019/20 iliyofanyika jana Julai 19, 2019 katika Kijiji cha Magoma, Kata Binagi wilayani humo.

Katika mdahalo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia ulioendeshwa kwenye kampeni hiyo, wazee hao walishindwa kuilaani mila ya ukeketaji baada ya mmoja wa wanajamii kutaka wageuza fimbo zao chini kama ishara ambao huwa wanaitumia kulaani jambo lolote baya katika jamii ya wakurya.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za watoto na wanawake KIVULINI, Yassin Ally (wa tatu kulia) akizungumza kwenye mdahalo huo huku akiwa ameshika fimbo ya mmoja wa wazee wa koo wilayani Tarime.
Mkuu wa Wilaya Tarime, Charles Kabeho (wa nne kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo awamu ya pili baada ya kutamatika kwa awamu ya kwanza mwaka 2017/18.
 Mkuu wa Wilaya Tarime, Charles Kabeho alisisitiza wanajamii wilayani Tarime kuachana na mila zenye madhara ikiwemo ukeketaji kwa wasichana huku wakiendeleza mila na desturi zinazochochea maendeleo katika jamii.
 Katibu Tawala wilayani Tarime akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Tarime, Ochieng Wayoga akieleza juhudi mbalimbali ikiwemo utoaji elimu zinazofanyika wilayani humo kupambana na mila potofu ikiwemo ukeketaji katika jamii.
 Wakazi wa Kata ya Binagi wilayani Tarime wakifuatilia mdahalo kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo.
 Mmoja wa waendesha bodaboda katika Kijiji cha Magoma akitoa msisitizo kwa bodaboda wenzake kuachana na tabia ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike kwa kuwahadaa na lifti.
 Mmoja wa wakazi wa Tarime akisisitiza wanajamii kuishi kwa amani badala ya kutendeana ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kwenye ndoa.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyasaricho wilayani Tarime wakitoa ujumbe wa kupambana na ukatili wa kijinsia kupitia nyimbo na ngojela.
 Kikundi cha ngoma za asili kutoka Tarime kikitumbuiza na kutoa ujumbe wa kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wilayani Tarime kwa mwaka 2019/2019.
 Viongozi wa Serikali na asasi mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa kampeni hiyo.
Kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Tarime ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango mkakati wa kitaifa unaolenga kupunguza aina zote za ukatili wa kijinsia hadi kufikia asilimia 50 katika kipindi cha mwaka 2017/2022.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.