LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vijana mkoani Mwanza wapania kuanzisha “Kijiji cha Vijana”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Vijana mkoani Mwanza wameadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani 2019 na kutoa msisitizo kwa Serikali kuendelea kuwaunga mkono ili kutekeleza kwa vitendo kauli ya Tanzania ya Viwanda.

“Tunaomba kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari moja kwa ajili ya kuanzisha Kijiji cha Vijana katika Mkoa wa Mwanza ili kutumia Kijiji hicho kama jukwaa la maendeleo na eneo rasmi la kila kijana kulitumia kwa shughuli za ubunifu na maendeleo ili kuinua uchumi” wameeleza vijana kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika viunga vya Gand Hall jijini Mwanza, Agosti 12, 2019
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Afisa Vijana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Diana Rwechungura akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
 Mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Dkt. Christopher Kadio akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani 2019 yaliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katika viunga vya Gand Hall jijini Mwanza.
 Mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Dkt. Christopher Kadio akikagua mabanda ya bidhaa mbalimbali za vijana kwenye maadhimisho hayo.
Viongozi na vijana kutoka taasisi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Dkt. Christopher Kadio (wa tano kushoto) huku wakiwa na vyeti walivyokabidhiwa baada ya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katikwa viunga vya "Gand Hall" wilayani Nyamagana.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.