LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Magu awakumbuka vijana "atumia zaidi ya shilingi milioni 30"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Mbunge wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, Boniventura Kiswaga (wa tatu kushoto) amekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 (Tsh. 31,950,000) kwa vijana wa kiume na kike jimboni humo ili kusaidia kukuza, kuendeleza na kuibua vipaji vya soka.

Kiswaga alitoa vifaa hivyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea Vijiji mbalimbali jimboni humo ili kusikiliza na kutatua kero na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwa wananchi katika Vijiji 82 ambapo kila Kijiji kilipata seti mbili za jezi na mpira mmoja wa miguu.
"Nawaomba mtumie vifaa hivi (mipira na jezi) vyema ili mjiimarishe kwani napenda kuona kila Kijiji kikiwa na timu bora na imara ili mpate fursa ya kushiriki mashindano mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa. Alisisitiza Kiswaga huku akiwakumbusha umuhimu wa michezo kuwa ni pamoja na kutoa fursa za ajira pamoja na kuimarisha afya.

Naye Afisa Michezo Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Kabula Malale alimshukuru na kumpongeza mbunge huyo kwa kukabidhi vifaa vya michezo katika Vijiji na taasisi mbalimbali ikiwemo Shule kwani vitaongeza kasi ya ukuaji wa soka kwa vijana wilayani Magu.

Baadhi ya vijana wakimshukuru mbunge wao kwa kutimiza ahadi alihuyotoa na kuahidi kuvitumia vyema ili kukuza vipaji vyao na hatimaye Wilaya Magu kuwa na timu bora itakayoshiriki michuano mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.