LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bashe aagiza wanunuzi wa pamba wilayani Misungwi kulipa madeni ya wakulima

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewataka wanunuzi wa pamba mbegu katika Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, kuhakikisha wanawalipa wakulima fedha zote wanazodaiwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) ili ziwasaidie kujiandaa na msimu mpya wa kilimo.


Bashe ametoa agizo hilo Septemba 28, 2019 wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la pamba wilayani Misungwi, kilichowajumuisha viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda, viongozi wa vyama vya Ushirika, Maafisa Kilimo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Wakuu wa Taasisi pamoja na Idara za Kilimo.

Kampuni zinazodaiwa na wakulima wilayani Misungwi ni BIRCHAD Group inayodaiwa Tsh. Milioni 334 pamoja na ICK ambayo imejitoa kununua pamba wilayani humo ikiwa na demi la Tsh. Milioni 405 na hivyo kufanya jumla ya fedha zote wanazodai wakulima kupitia AMCOS zao kuwa Tsh. Milioni 739.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akitoa maelekezo kwenye kikao baina yake na viongozi mbalimbali wilayani Misungwi wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda, viongozi wa vyama vya Ushirika, Maafisa Kilimo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Wakuu wa Taasisi pamoja na Idara za Kilimo.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (katikati) akizungumza kwenye kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda na kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya Misungwi, Latifa Malimi.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (wa tatu ksuhoto) akizungumza kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Emil Kasagala, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Antony Bahebe, Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda, Katibu wa CCM Wilaya Misungwi, Latifa Malimi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Upendo Naftali.
 Afisa Kilimo na Ushirika Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Majid Kabyemelwa akitoa taarifa ya hali ya pamba wilayani Misungwi.
 Mwakilishi wa kampuni ya ununuzi wa pamba wilayani Misungwi ya BIRCHAD Group, Arshard Jetha ambaye ni Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo akitoa uhakika wa kununua pamba yote iliyo kwa wakulima kupitia AMCOS zao.
 Mmoja wa viongozi wa AMCOS wilayani Misungwi akieleza madeni wanayodai wanunuzi wa pamba wilayani humo.
 Mhasibu wa AMCOS ya Ibongoya wilayani Misungwi, Elizabeth Zephania akieleza hali ya ununuzi wa pamba ilivyo katika AMCOS hiyo.
 Viongozi mbalimbali wakifuatilia kikao hicho.
 Viongozi na Watendaji mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
 Viongozi kutoka AMCOS mbalimbali wilayani Misungwi wakiwa kwenye kikao hicho.
 Kikao baina ya Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na viongozi mbalimbali kilimo wilayani Misunwgi.
 Awali Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi, Antony Bahebe baada ya kuwasili wilayani Misungwi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akisalimiana na  Katibu Tawala Wilaya Misungwi, Peter Sabatho.
Awali Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (kulia) akitoa taarifa ya hali ya kilimo wilayani humo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.