LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hospitali ya Bugando yaanza utekelezaji agizo la JPM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando Profesa Abel Makubi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa ulioanza Septemba 15, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Rais Dkt. John Pombe.

Judith Ferdinand, BMG
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Katoliki Cha Afya na Sayansi Bugando (CUHAS), imeanza kufanya utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani, moyo, kisukari, figo na shinikizo la damu (blood pressure).

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Julai 15, 2019 alipokuwa akizindua miradi tiba hospitalini hapo ambapo aliitaka hospitali hiyo kuundwa tume ya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza huku Wizara ya Afya ikisimamia zoezi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 15, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando Prof.Abel Makubi alisema utafiti huo kwa hatua ya awali utagharimu milioni 60 ingawa gharama zinaweza kuongezeka pindi mchakato wa kuchunguza (kuchambua) utakapo fanyika ambapo utafanyika katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Mara na Shinyanga ikiwa ni Wilaya 12 ukitarajiwa kuwafikia wananchi 7,000.

Prof. Makubi alisema ili kujiridhisha ukubwa wa tatizo na dalili za awali za magonjwa hayo utafiti huo ambao umeanza Septemba 15, 2019 utakamilika kwa siku 14 na baada ya hapo utafanyika uchambuzi kwa miezi mitatu ambao umelenga ngazi ya chini kuanzia Kaya hadi Kijiji.

Pia aliwaomba wananchi wa Kanda ya Ziwa ambao utafiti utafika kwao watoe ushirikiano ambapo watapimwa magonjwa hayo kwa hiari.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi CUHAS ambaye ni Mratibu wa Utafiti huo Dkt.Anthony Kapesa alisema umeshirikisha madaktari bingwa 12 kati ya hao wawili watajishughulisha na upimaji wa magonjwa ya moyo huku 10 wakihusika na tiba na utafiti ambapo watashirikiana na timu ya watafiti wasaidizi zaidi ya 200 waliopewa mafunzo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.