LIVE STREAM ADS

Header Ads

Michuano ya Kalemani Cup 2019 yahitimishwa kwa kishindo Chato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Michuano ya soka ya kombe la mbunge wa jimbo la Chato mkoani Geita ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani maarufu kama Kalemani Cup 2019, imefikia tamati kwa timu ya Buselesele kuibuka kidedea baada ya kuitandika kwa mikwaju ya penati (3-2) timu ya Kibehe kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Faina ya michuano hiyo iliyoanza Juni 20, 2019 kwa kushirikisha timu 115 kutoka Vijiji vyote wilayani Chato ilipigwa Septemba 15, 2019 katika uwanja wa Magufuli Square Mjini Chato ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel huku ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mlinda mlango wa timu ya Kibehe akiokoa mpira kutoka kwa mshambuliaji wa timu ya Buselesele.
 Timu ya Buselesele (kushoto) pamoja na Kibehe (kulia) zikiwa tayari kuanza mchezo wa fainali.
 Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akisalimiana na waamuzi wa mchezo huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa timamu kufuatilia mchezo wa fainali kwenye michuano ya Kalemani Cup 2019 Mjini Chato.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.