LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Magufuli ataka uchunguzi zaidi “vifo vya Saratani Kanda ya Ziwa”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufanya utafiti ili kubaini sababu za wagonga wengi wa Saratani nchini wanatokea mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Rais Dkt. Magufuli aliyasema hayo Julai 15, 2019 wakati akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua rasmi wa huduma za tiba ya Saratani, upanuzi wa vyumba vya upasuaji, maabara ya kisasa ya Molecular Baiolojia, upanuzi wa jengo la wagonjwa wa dharura na mahututi, ufunguzi jengo la wagonjwa wanachama wa NHIF, mtambo wa kuzalisha Oksijeni ya wagonjwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya mishipa ya damu (Dripu) katika Hospitali ya Bugando.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.