LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maboresho katika skimu ya umwagiliaji Dakawa Morogoro yaleta tija kwa wakulima

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Maboresho ya skimu ya umwagiliaji katika skimu ya Dawawa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro yamesaidia wakulima wadogo wa kilimo cha mpunga kuongeza mavuno yao kutoka tani 600 hadi zaidi ya tani 13,000 kwa hekta moja. 

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakulima kwenye skimu hiyo baada ya kutembelewa na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliajia waliofika kwenye skimu hiyo kujionea maboresho yanayofanyika kwa ufadhili wa wadau mbalimbali ikiwemo USAID.
#BMGHabari
Mkulima Bertha Chilosa kutoka ushirika wa waakulima wadogo wa kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya umwagiliaji Dakawa (Uwawakuda) wilayani Mvomero akibainisha namna skimu hiyo ilivyoongeza manufaa kwa wakulima.
Wakulima kutoka chama cha wakulima wadogo wa kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya umwagiliaji Dakawa (Uwawakuda) iliyopo wilayani Mvomero wakiwa kwenye kikao cha pamoja na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliajia na wahandisi wa kampuni ya ujenzi ya NORPLAN Tanzania Ltd iyoyejenga miundombinu katika skimu hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.