LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bugando kuwaondolea adha wakazi wa Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza, Prof. Abel Makubi amesema utoaji huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani katika hospitali hiyo, umesaidia kuondoa adha kwa wagonjwa waliokuwa wakienda jijini Dar es salaam kusaka matibabu hayo.

Prof. Makubi aliyasema hayo Julai 15, 2019 wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma za tiba ya Saratani, upanuzi wa vyumba vya upasuaji, maabara ya kisasa ya Molecular Baiolojia, upanuzi wa jengo la wagonjwa wa dharura na mahututi, ufunguzi jengo la wagonjwa wanachama wa NHIF, mtambo wa kuzalisha Oksijeni ya wagonjwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya mishipa ya damu (Dripu) ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando, Mhashamu Baba Askofu Renatus Kwande akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.