LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watanzania watakiwa kuiheshimu sekta ya Ubaharia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhadhiri Msaidizi wa Ufundi Meli kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Mhandisi Latifa Mzara (kushoto) juu ya namna wanavyofanya shughuli. Ni baada ya kutembelea banda la chuo hicho katika ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Usafiri kwa njia ya Maji yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.

Judith Ferdinand, BMG
Taaluma ya ubaharia ni sekta nyeti na ya kitaalamu hivyo wanajamii nchini wameaswa kuiheshimu na kubadili mtazamo hasi ambao umekuwa ukitazamwa na baadhi yao kana kwamba ni sekta ya watu wasio na maadili.

Hii ni baada ya hivi karibuni kuibuka msemo wa baharia miongoni mwa wanajamii na kulitumia vibaya jina hilo ambalo linaonekana kama ni kundi fulani la kihuni.

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (National Institute of Transport - NIT) Mhandisi Latifa Mzara aliyasema hayo Septemba 25, 2019 kwenye maadhimisho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Septemba 23-26, 2019.

Aidha Mhandisi Mzara alitumia fursa hiyo kuhimiza wanajamii kuwaruhusu na kuwapa hamasa watoto wa kike kusoma masomo yanayotokana na sekta hiyo ikiwemo ya ufundi wa meli kwani ni nyeti na nguzo ya uchumi.

"Nawaomba wazazi wawahamasishe watoto wao hususani wa kike kusoma masomo ya ubaharia kwani kuna fursa nyingi katika sekta hii na ikumbukwe kuwa hii ni kazi muhimu kama ilivyo kazi nyingine"alisema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Chama Cha Mabahari Tanzania (TASU) Mkoa Dar es salaam, Abdul Mgeni alisema kazi ya chama hicho ni kutetea mabaharia pale wanapopatwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maslahi yao.

No comments:

Powered by Blogger.