LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watumishi mkoani Mwanza waomba Serikali kushughulikia maombi yao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Chama cha watumishi wa Serikali (TUGHE) Mkoa Mwanza kimeomba suala la upandaji madaraja kuzingatiwa kwani kutofanya hivyo kunashusha ari ya utendaji kazi kwa wafanyakazi.

Mwenyekiti wa chama hicho, Aloysius Mapembe aliyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa kazi wa chama hicho uliofanyika jijini Mwanza na kuongeza kwamba mtumishi anapofanya kazi kwa muda mrefu bila kuboreshewa maslahi ama kupandishwa cheo hupunguza morali ya kufanya kazi kwa ufasaha.

Naye Katibu wa TUGHE Mkoa wa Mwanza, Amini Msambwa alisema matamko mengi yamekuwa yakitolewa kuhusu suala la upandaji wa madaraja kwa watumishi lakini utekelezaji umekuwa hauzingatiwi kwa wakati ama wakati mwingine kubagua baadhi ya watumishi.

"Unakuta watumishi hawa hawa ambao walitangulia kuajiriwa hawajapandishwa daraja huku aliye anza kazi juzi juzi anapandishwa, mgeni rasmi kwa kuwa wewe ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza, tunaomba utusaidie, tatizo kubwa lipo kwa maafisa utumishi wetu kwani wamekuwa na kasi ndogo na haitoshi" alisema Msambwa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio aliipongeza TUGHE kwa kuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wanachama wake huku akiwahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa bidii wakati Serikali ikiendelea kuboresha maslahi yao.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.