TCRA yaja na mwarobaini usajili wa laini za simu kwa alama za vidole
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na watoa huduma za mawasiliano ya simu, imeanzisha
kampeni maalum ya usajili wa laini za simu kwa njia ya vidole ili kuwafikia wananchi
wengi kabla ya mwisho wa zoezi hilo Disemba 31, 2019.
Akizungumza Septemba
27, 2019 na waandishi wa habari jijini Mwanza, Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi
Francis Mihayo amesema kampeni hiyo itaongeza kasi ya usajili wa laini za simu
kwa alama za vidole na hivyo kuwafikia wananchi wengi wakiwemo wa visiwani.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: