LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella ahamasisha wananchi kushiriki zoezi la uandikishaji wapiga kura

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 limeanza kote nchini ambapo kwa Mkoa Mwanza zaidi ya wananchi Milioni moja wanatarajiwa kujiandikisha.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella pia ametumia fursa hiyo kujiandikisha katika Mtaa wake wa Kiseke PPF uliopo Manispaa ya Ilemela huku akitoa hamasa kwa wananchi wenye umri wa kuanzia miaka 18 kujitokeza mapema ili kujiandikisha badala ya kusubiri siku ya mwisho.

Zoezi hilo litanatarajiwa kudumu kwa muda wa siku saba hadi Oktoba 14, 2019 huku Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.