LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaruhusu shughuli kuendelea katika machimbo ya Shilalo wilayani Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Madini, Doto Biteko Oktoba 17, 2019 ameruhusu shughuli za uchimbaji dhahabu kuendelea katika machimbo ya Shilalo yaliyopo katika Wilaya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na mvutano uliokuwepo.

Oktoba 07, 2019 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alisitisha uchimbaji dhahabu katika maduara 38 kati 57 ili kutafuta mwafaka wa mgogoro wa umiliki wa ardhi uliokuwepo ambapo baada ya maamuzi hayo, Serikali itaandaa utaratibu mzuri wa kusimamia machimbo hayo ili pande zote zinufaike.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye mkutano baina ya Waziri wa Madini na wachimbaji wadogo wa dhahabu Shilalo wilayani Misungwi.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa Wilaya Misungwi Juma Sweda (kulia), Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi Kisena Mabuba (katikati) pamoja na Afisa Tarafa ya Inonelwa Glory Kaywanga (kushoto) wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.