LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko asisitiza "bei ya makaa ya mawe haitaongezeka"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waziri wa Madini, Doto Biteko amesisitiza kwamba bei ya ununuzi wa makaa ya mawe haitaongezeka zaidi ya bei elekezi ya Serikali.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Oktoba 14, 2019 jijini Mwanza alipokutana na wanunuzi wa madini hayo kutoka makampuni ya Tanga Cement, Lake Cement pamoja na KEDA (Tanzania) Ceramics wanaotumia madini hayo kama nishati ya viwandani kwa ajili ya uzalishaji wa saruji na vigae vya majumbani.

Hatua hiyo inatokana na wanunuzi wa makaa ya mawe nchini kuwa na mvutano wa bei baina yao na kampuni ya TANCOAL inayowauzia madini hayo.

Mvutano huo ulianza baada ya Serikali kuitaka kampuni ya TANCOAL kulipa deni la Tsh. Bilioni 23.9 ambazo ni mrabaha wa mauzo na usafirishaji wa makaa ya mawe pamoja na adhabu ya asilimia 50 kuanzia Septemba mwaka 2011 hadi Juni 2019 ambapo kampuni hiyo ilitaka kuongeza bei ya madini hayo ili kufidia gharama za deni hilo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa Mwanza.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.