LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vijana wa Halaiki wanogesha sherehe za Mwenge wa Uhuru, kifo cha Baba wa Taifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Vijana wa Halaiki wameonesha ubunifu wa hali ya juu katika kuonesha maumbo mbalimbali ikiwemo ramani ya Taifa kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana pamoja na kumbukizi ya miaka 20 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarageb Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, Oktoba 14, 2019 mgeni rasmi akiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu Ndugu Mzee Mkongea Ally kwenye sherehe za kilele za mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika uwanja wa michezo Ilulu Mjini Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa jukwaa kuu na viongozi wengine wa kitaifa kwenye sherehe hizo.
Wabunge wa Mkoa wa Lindi na viongozi wengine wakiserebuka na msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama "Harmonize".
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakiserebuka na msanii Harmonize.
Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo.
Umbo la ukaribisho.
Ramani ya Taifa
Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali.
Vijana wa Halaiki wakichora maumbo mbalimbali.
Vijana wa Halaiki.
Kikundi cha utamaduni cha Dege la Jeshi kikitumbuiza kwenye sherehe hizo.
Wanenguaji wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) wakitumbuiza.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kala Jeremiah akitumbuiza kwenye sherehe.
Picha na IKULU ya Tanzania

No comments:

Powered by Blogger.