LIVE STREAM ADS

Header Ads

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza yapata mlezi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa Mwanza (MPC), ni Klabu iliyosajiliwa chini ya Sheria ya "Society Act" tarehe 09 Disemba 1994 kwa usajili wa namba S.109 kufanya kazi ndani ya Mkoa Mwanza lengo kuu likiwa ni kuchochea maendeleo ya Mkoa Mwanza.

Ndugu wanachama wa MPC, Kamati Tendaji ya Klabu inapenda kuwataarifu kuwa, kwa sasa  Klabu yetu imempata mlezi ambaye atahusika na suala zima la kuilea na kuishauri Klabu kwa muda wote kama neno tafsiri ya "Mlezi" lilivyo.

Mlezi huyo ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella ambaye pia ni mdau mkubwa wa masuala ya Habari na Vyombo vya Habari Tanzania.

Hatua hiyo imetokana na ziara iliyofanywa na viongozi wa Klabu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Oktoba 11, 2019.

Hivyo tunamshukuru Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. John Mongella kwa kukubali kuwa mlezi wa Klabu yetu.

Imetolewa na Kamati Tendaji MPC tarehe 11.10.2019
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko (kushoto) akimshuku Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) baada ya kukubali kuwa mlezi wa chama hicho. kulia ni Makamu Mwenyekiti MPC, Albert Sengo.
#BMGHabari

No comments:

Powered by Blogger.