LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shule ya Msingi Little treasures yafanya Sherehe na Maombi baada ya matokeo mazuri

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo Manispaa ya Shinyanga imefanya sherehe ya kujipongeza iliyoambatana na maombi ya shukrani kwa kupata matokeo mazuri katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2019 wakiongoza na kauli mbiu 'Tanzania Four, Shinyanga One".

Shule ya Little Treasures imeshika nafasi ya nne katika orodha ya shule 10 bora kitaifa huku mwanafunzi Daniel Ngassa kutoka shule hiyo akishika nafasi ya saba kwenye orodha ya watahiniwa bora kitaifa na wanafunzi wengine wawili ambao ni Suzane Assenga pamoja na Scolastica Shelembi wakiingia kwenye orodha ya watahiniwa 10 bora kitaifa upande wa wasichana.

Sherehe ya pongezi na maombi kwa shule hiyo imefanyika Oktoba 19,2019 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohamed Kahundi, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, wazazi na walezi, walimu na wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2019.

Mkurugenzi wa Shule hiyo, Lucy Dominic alisema imeshika nafasi ya nne kitaifa, ya kwanza katika wilaya ya Shinyanga na ya kwanza katika Mkoa wa Shinyanga hivyo lengo la sherehe na maombi hayo ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda na kuiinua shule hiyo.

"Tuko hapa kwa lengo kuu la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kuiinua shule yetu. Tunaamini kuwa ni Mungu pekee anaye tuwezesha, ni nafasi pia kuendelea kuomba Neema zake azidi kutubariki zaidi na zaidi kwani sisi kama wanadamu tunajua tulikotoka na tulipo lakini hatujui tunakokwenda na ndiyo maana tunamtanguliza mbele azidi kuwa Nuru yetu" alisema Dominic na kuongeza;

"Tumekutana hapa ikiwa ni mwendelezo wa furaha isiyo kifani kwetu wanafamilia ya Little Treasures ili kumshukuru Mungu na kusherehekea mafanikio makubwa tuliyoyapata katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2019" alifafanua.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi aliipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 na kuahidi kutoa zawadi kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani.

"Little Treasures mmefanya maajabu, tunawapongeza sana, mmeutangaza Mkoa wetu, mmeuingiza Mkoa wetu katika shule 10 bora kitaifa" alisema Kahundi na kuongeza;

"Nazipongeza Shule zetu tatu binafsi ambazo ni Little Treasures, Kwema Modern na Rocken Hill kwa kweli zimetangaza mkoa wetu kwa matokeo mazuri kitaifa. Lakini nizipongeze Shule za Serikali za Mkoa wa Shinyanga ambazo zimefanya vizuri kwenye matokeo haya nazo ni Kinaga iliyopo Kahama, Ilobi iliyopo Kishapu na Mwenge iliyopo Manispaa ya Shinyanga" alisema Kahundi.

Mkoa wa Shinyanga ulishika nafasi ya nafasi ya 15 mwaka 2018 kwenye matokeo ya darasa la saba ambapo mwaka huu 2019 umeshuka kwa nafasi mbili hadi nafasi ya hadi nafasi ya 17.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa sherehe hiyo.
Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Little Treasures,  Lucy Dominic akitoa taarifa ya Shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi 91 waliomaliza darasa la saba katika shule hiyo na wote wamepata daraja A katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2019.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akicheza na wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2019.
Baadhi ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi Little Treasures mwaka 2019.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Msingi Little Treasures, Tilulindwa Sulusi akimtambulisha mwanafunzi aliyeshika nafasi ya saba kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019, Daniel Ngassa.
Baadhi ya waalikwa wakifuatilia shughuli hiyo.
Wazazi wa Daniel Ngassa wakimpongeza kijana wao kwa kushika nafasi ya saba kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019.
Nabii Janeth Aminiel Kimo wa Kanisa la Uwezo wa Bwana Mwanza akiomba wakati wa shehere hiyo.
Askofu Raphael Machimu (kulia) kutoka Kanisa la EAGT Shinyanga akiendesha maombi ya shukrani.
Maombi yakiendelea kumshukuru Mungu 
Padre Tupendane Philemon wa Kanisa Katoliki la Mt. Yosefu Mipa (Jimbo Katoliki la Shinyanga) akiwaombea wahitimu wa shule ya msingi.
Maalim/ Ustadhi Ashiraf Majaliwa akitoa salamu za Mufti wa Tanzania, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na kuomba dua kwa ajili ya shule ya Little Treasures.
Watahiniwa bora kitaifa matokeo ya mtihani darasa la saba 2019 kutoka Shule ya Msingi Little Treasures (Daniel Ngassa katikati aliyeshika nafasi ya saba kitaifa) na wanafunzi wa kike ambao ni miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019 Suzane Assenga (kulia) na Scolastica Shelembi (kushoto) wakikata keki. 
Wahitimu darasa la saba 2019 Shule ya Little Treasures wakicheza wimbo wa Yope wa Diamond na Innoss'B.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Kiondo akizungumza wakati wa sherehe na maombi kwa shule ya hayo.
Meneja wa Shule ya Msingi Little Treasures, Wilfred Mwita akizungumza wakati wa shughuli hiyo.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga, Neema Mkanga akitoa salamu zake.
Zoezi la kukabidhi keki likiendelea. 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog

No comments:

Powered by Blogger.