LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maadhimisho ya Siku ya Akiba Duniani 2019 yafanyika jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Shirika la SBFIC tawi la Tanzania (Savings Banks Foundation for International Coorperation), limeungana na wadau pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo Benki ya Akiba (Akiba Commercial Bank- ACB), kuadhimisha Siku ya Akiba Duniani 2019.

Maadhimisho hayo yamefanyika Oktoba 26, 2019 katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalila amehimiza umuhimu wa utoaji elimu ya akiba katika jamii.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Wilaya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt. Severine Lalika akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la SBFIC (Savings Banks Foundation for International Coorperation) tawi la Tanzania, Stephen Safe akizungumza kwenye maadhimisho
 Mkuu wa Idara ya Masoko Benki ya Akiba, Dorah Saria akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo.
 Meneja Masoko kutoka Mfuko wa Self Microfinance, Linda Mshana akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Kaimu Mrajisi Msaidizi Uhamasishaji na Uratibu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Petronila Shirima akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Idara ya Masoko Benki ya Akiba, Dorah Saria (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalila (kulia) kibubu kinachotumika kuwajengea watoto uwezo wa kutunza akiba wangali bado wadogo.
 Mkurugenzi wa Shirika la SBFIC, Stephen Safe akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalila (kulia) flana maalum ya Siku ya Akiba Duniani 2019.
 Meneja wa Benki ya Akiba Mkoa Mwanza, Hariet Bujiku (wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine Lalika (kushoto).
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.