Tamasha la Urithi kutikisa jijini Mwanza kwa siku tatu mfululizo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kwenye kilele cha Tamasha la Urithi (Urithi Festival 2019)
litakalofanyika katika viunga vya Rock City Mall jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella ameyasema hayo Oktoba 29, 2019 wakati akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari kuhusiana na tamasha hilo litakalofanyika kwa siku tatu
mfululizo kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 02, 2019.
Tamasha la
pili la Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania (Urithi Festival) lilizinduliwa rasmi
Septemba 22, 2019 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia
Suluhu Hassan jijini Dar es salaam na kisha kuzunguka mikoa mbalimbali nchini
kabla ya kuhitimishwa jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa taarifa kuhusu tamasha la Urithi 2019 litakalofanyika jijini Mwanza.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
SOMA>>> Habari za matamasha mbalimbali
No comments: