LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mahafali ya kidato cha nne KOM SEKONDARI yafana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi ameongoza sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom "Kom Secondary) iliyopo Butengwa katika Manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 189 kati yao wasichana 80 wavulana 109 wamehitimu elimu ya kidato cha nne.

Mahafali hayo yalifanyika Novemba 16, 2019 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya wazazi,wageni waalikwa,wanafunzi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

"Nimeambiwa kuna baadhi ya wazazi wanachelewa kulipa ada.Niwakumbushe tu kuwa ukimpeleka mtoto katika shule binafsi maana yake una uwezo wa kulipa ada, sasa lipeni. Elimu ni gharama, hata kwenye shule za Serikali (Public Schools) kuna gharama, kuna nguvu za wananchi" alisema Kahundi.

Afisa Elimu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuwakatia bima ya afya watoto wao ili kurahisisha matibabu pindi wanapougua. 

"Vijana mnarudi nyumbani mnatakiwa kuwa watii kwa wazazi wenu,nanyi wazazi msijaribu kuwaozesha wanafunzi hawa waliohitimu kidato cha nne.Msiende kuozesha watoto hawa" alisema Kahundi. 

Awali Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi alisema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 wanafunzi 179 walihitimu kati yao 167 walijiunga na kidato cha tano.

Aidha kwa kipindi cha miaka 10 kati ya mwaka 2009 hadi 2018,Koyi alisema jumla ya wanafunzi 1420 wamehitimu kidato cha nne kati yao wanafunzi 1093 walichaguliwa kuendelea na kidato cha tano.

Alisema wanafunzi waliobaki 327 wengi wao walijiunga na vyuo mbalimbali vikiwemo vya uhasibu, biashara,ualimu, uuguzi, sheria huku akibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na walimu darasani pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya wanafunzi.

Akisoma taarifa ya shule, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba alisema shule hiyo iliyosajiliwa mwaka 2006 ikiongozwa na kauli mbiu "Elimu bora kwa wote – Quality Education for All" akiongeza kwamba shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 579 kati yao wavulana ni 314 na wasichana 265 huku walimu wakiwa ni 32 hivyo uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:18.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji zinazosababishwa na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha, baadhi ya wazazi kutolipa ada kwa wakati hivyo kuwafanya watoto wachelewe kufika shule inapofunguliwa na baadhi ya watoto kutowalipia watoto wao bima ya afya. 
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akikata utepe kwenye kuashiria kuanza kwa mahafali hayo.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akiwasalimia wazazi na wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiingia ukumbini.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa salamu wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba akisoma historia ya shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikata keki maalumu wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikabidhi zawadi ya keki kwa walimu wa shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom.
Wazazi, walezi na wageni mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
Vijana wakionesha ubunifu wa mavazi ya Mama Afrika wakati wa Mahafali hayo.
Vijana wa Skauti wakionesha michezo ya ukakamavu.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom ambapo makadirio ya gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo ni milioni sita.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akichangia pesa wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara shule ya sekondari Kom.
Wasaa wa kugawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne 2019 katika shule ya Sekondari Kom.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Walimu wa shule ya sekondari Kom wakikabidhi zawadi kwa Mgeni rasmi ,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi.
Imeandaliwa na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog

No comments:

Powered by Blogger.