LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tuzo za Cheza Kidansi kutolewa Disemba 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Tuzo za Muziki wa Dansi Tanzania zilizopewa jina la Cheza Kidansi Awards 2019 zinatarajiwa kutolewa jijini Mwanza Disemba 21, 2019 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Mratibu Mkuu wa tuzo hizo, Bernard James anasema tuzo hizo zitatolewa katika ukumbi wa Bundasliga jijini Mwanza zikihusisha vipengele 11 ambavyo ni mwanamuziki bora, wimbo bora, video bora, rapa bora, mwanamuziki chipukizi, mpiga chombo bora, mtunzi bora, mwanamuziki bora kutoka Congo ambapo kila kipengele kitakuwa na nafasi ya watu wanne ambao watachuana na watapigiwa kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi pamoja na mitandao ya kijamii.

Ujio wa tuzi hizo chini ya kampuni ya Cheza Kidansi Intertainment ni sehemu ya kutambua mchango na jitihada zinazofanywa na wanamuziki wa dansi nchini Tanzania ambao wamekuwa na mchango mkubwa wa kuelimisha na kuburudisha jamii.
Imeandaliwa na Judith Ferdinand, BMG
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.