RC Mongella azindua mradi mkubwa wa maji katika Shule za Lake Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mradi huo
umefadhiliwa na taasisi ya kidini ya “Siri Guru Singh Sabha Mwanza” ukielezwa
kwamba utaleta manufaa makubwa ikiwemo kupunguza gharama za ankra za maji ambazo
kwa mwezi zilikuwa kati ya shilingi milioni tatu hadi milioni tano kwa mwezi.
Akizungumza
na uongozi pamoja na wanafunzi wa Shule za Lake kabla ya kuzingua mradi huo Novemba 16, 2019 Mongella ametaka Shule hiyo kurejea kwenye enzi zake ambapo ilikuwa ikifanya
vizuri katika mitihani ya kitaifa ili kuendana na sifa yake ya kutoa wanafunzi
bora ambao sasa ni viongozi mashughuli nchini akiwemo Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye hafla.
Meneja wa Shule za Lake Mwanza, Jagdish Mehta akitoa salamu kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa Bodi ya Wamiliki pamoja na wafadhili kutoka taasisi Siri Guru Singh Sabha Mwanza.
Wazazi, waalimu na wanafunzi wakifuatilia hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tano kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiweka jiwe la msingi kwenye mradi huo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionja maji ya kisima hicho ambayo ni safi na salama.
SOMA>>> Mkusanyiko wa habari mbalimbali
No comments: