LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza afungua Mkutano wa Marafiki wa Habari


Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amefungua mkutano wa wasaa wa marafiki wa Habari mkoani Mwanza ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Habari Mkoa Mwanza (MPC).

Akifungua mkutano huo Novemba 09, 2019 jijini Mwanza, Mongella alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari hivyo itaendelea kushirikiana na wabahabari katika kuchochea maendeleo.

Aidha Mongella aliipongeza MPC kupitia Mwenyekiti wake Edwin Soko kwa kuandaa mkutano akisema utasaidia kujadili fursa mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo ukarabati na ujenzi meli mpya katika Ziwa Victoria pamoja na ujio wa reli ya kisasa (SGR) huku ukitoa picha halisi katika kuelekea kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Biashara mkoani Mwanza utakaofanyika mwaka ujao.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko alisema mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano baina ya vyombo vya habari na wadau katika kufanikisha ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza huku akisisitiza wanahabari kufanya kazi kwa weledi ili kulinda mustakabali wa amani kwa Taifa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa salami za ufunguzi kwenye mkutano huo.
Wanahabari na marafiki wa habari wakifuatilia mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.