LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Ndalichako azindua Ofisi Misungwi "awapa rungu Wakuu wa Wilaya na Mikoa"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezindua jengo jipya la Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Elimu Wilaya Misungwi mkoani Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchini kuweka mikakati ya pamoja ya kupambana na utoro katika Shule za Msingi na Sekondari.

Waziri Prof. Ndalichako alifanya uzinduzi huo Novemba 09, 2019 ambapo ofisi hiyo ni miongoni mwa ofisi 100 za Udhibiti Ubora wa Elimu zinazojengwa katika Halmashauri mbalimbali nchini.
#BMGHabari
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Elimu Wilaya Misungwi mkoani Mwanza. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Kisena Mabuba (wa pili kushoto).
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.