LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza akabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) amekabidhi hati ya umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba 6,500k wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (The Open University of Tanzania) katika eneo la Mkolani jijini Mwanza na kutoa mwezi mmoja uongozi wa Chuo hicho kuandaa mpango wa kuendeleza ardhi hiyo.

Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kituo cha Mwanza, alikabidhi hati hiyo Novemba 09, 2019 baada ya Serikali kufanya mabadiliko ya umiliki wa ardhi ambayo awali ilikuwa ikiimiliki na kuikabidhi kwa Chuo hicho.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kuahoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Chuo Kikuu Huria Tanzania akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Alex Makulilo (kulia).
 Awali majengo na hati ya umiliki wa ardhi hiyo katika eneo la Mkolani jijini Mwanza ilikuwa mali ya Serikali.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Chuo Kikuu Huria Tanzania akisisitiza jambo wakati wa zoezi la kukabidhi hati hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Chuo Kikuu Huria Tanzania akizungumza kabla ya kukabidhi hati hiyo.
 Mkuu wa Wilaya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt. Severine Lalika akitoa salamu zake akiwa ni mmoja wa wanazuoni waliosoma Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Alex Makulilo akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho.
 Wanazuo wa Chuo Kikuu Huria Tanzania wakifuatilia zoezi la Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kukabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa Chuo hicho katika Kata ya Mkolani jijini Mwanza.
 Wanazuoni wa Chuo Kikuu Huria Tanzania wakifuatilia zoezi hilo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.