LIVE STREAM ADS

Header Ads

Halmashauri ya Misungwi yapiga hatua usimamizi wa miradi ya maendeleo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha (wa tatu kulia) ameeleza kufurahishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, kufuatia miradi hiyo kusimamiwa kwa ufanisi mkubwa na thamani ya fedha kuonekana.

Naibu Nasha aliyasema hayo Jumamosi Julai 06, 2019 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mdhibiti Ubora Elimu Wilaya Misungwi ambapo Serikali ilitoa shilingi Milioni 152 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ulioanza Mei 25, 2019.

Kutokana na usimamizi mzuri wa mradi huo ambao umefikia hatua ya upauaji, kiasi cha fedha kilichotumika ni shilingi milioni 60 hivyo matarajio ni salio kubaki na hivyi kusaidia utekelezaji wa mradi mwingine kulingana na maelekezo yatakayotolewa ambapo hatua hiyo imetokana na gharama za ujenzi kupungua baada ya mfumo wa "Force Account" unaoshirikisha pia nguvu za wananchi kutumika.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha (wa pili kushoto) akisalimiana na Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Misungwi, Mwl. Diana Kuboja pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri hiyo baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara fupi ya kikazi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akiwasilisha taarifa fupi kuhusiana na hali ya elimu wilayani humo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akizungumza na watendaji mbalimbali Halmashauri ya Misungwi kabla ya kutembelea ujenzi wa jengo la Mdhibiti Ubora Elimu Wilaya Misungwi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akifika kwenye ofisi ya sasa ya Mdhibiti Ubora Elimu wilayani Misungwi ambapo alijionea ufinyu wa ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha alifika kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mdhibiti Ubora Elimu wilayani Misungwi na kuridhishwa na ujenzi huo.
Mdhibiti Ubora Elimu wilayani Misungwi, Mwl. Faustine Salala akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mdhibiti Ubora Elimu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha (wa tatu kulia) akifafanua jambo baada ya kutembelea jengo la Ofisi ya Mdhibiti Ubora Elimu wilayani Misungwi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akizungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Misungwi wakiwemo Waalimu Wakuu pamoja na Waratibu Elimu wilayani humo.
Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mdhibiti Ubora Elimu wilayani Misungwi unaendelea kwa kasi.
Ujenzi umefikia hatua hii ya upauaji.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.