LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella akagua miradi ya maendeleo Sengerema "milioni 400 zimeishaje"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Julai 04, 2019 alifanya ziara ya kukagua miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo wilayani Sengerema ikiwemo upanuzi wa Kituo cha Afya Katunguru ambacho alisisitiza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wilayani Sengerema akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwl. Emmanuel Kipole (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri Magesa Mafuru (wa kwanza kulia) kuhakikisha Kituo cha Afya Katunguru kinakamilika.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliofika Kituo cha Afya Katunguru kupata huduma za afya.
Jengo jipya la kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Katunguru. Kushoto ni chumba cha zamani kilichokuwa kinatumika kama jengo la kuhifadhia maiti kituoni hapo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella  akiwa na viongozi mbalimbali kukagua majengo mapya katika Kituo cha Afya Katunguru.
Sehemu ya majengo mapya katika Kituo cha Afya Katunguru.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ujenzi wa majengo katika Kituo cha Afya Katunguru.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ujenzi wa majengo katika Kituo cha Afya Katunguru.
Moja ya jengo jipya katika Kituo cha Afya Katunguru wilayani Sengerema.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella pia alikagua zoezi la ukusanyaji pamba katika AMCOS ya Kasenyi wilayani Sengerema.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wilayani Sengerema.
Pia Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ujenzi wa jengo la wazazi katika Kituo cha Afya Kasenyi wilayani Sengerema.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua pia zoezi la ukusanyaji pamba katika AMCOS ya Nyamazugo wilayani Sengerema na kusisitiza kwamba wakulima wataanza kulipwa fedha zao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwasili kukagua ujenzi wa Hospitali ya Buchosa inayojengwa kwa hadi ya Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Ujenzi katika Hospitali ya Buchosa unaendelea kwa kasi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ujenzi wa shimo kubwa la kuvunia maji katika Hospitali Buchosa.
Sehemu ya majengo mapya katika Hospitali ya Buchosa.
Ujenzi huu unaelekea ukingoni kukamilika.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ujenzi wa majengo mbalimbali katika Hospitali ya Buchosa wilayani Sengerema.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.