Header Ads

Mashauri mengi ya ukatili wa kijinsia kufutwa, polisi Nyamagana wachukua hatua

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Inaelezwa kwamba mashauri mbalimbali yanayohusiana na matukio ya ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, yamekuwa yakikosa mafanikio mahakamani na hivyo kufutwa kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ukosefu wa ushahidi.

Takwimu zinaonyesha kwamba mwaka jana 2018 kuanzia mwezi Januari hadi Disemba kulikuwa na mashauri 48 yaliyofikishwa mahakamani, lakini ni mashauri 14 pekee yaliyofikia hatua ya maamuzi huku mashauri 34 yakifutwa.

Aidha kwa mwaka huu 2019 kuanzia mwezi Januari hadi Juni, mashauri 23 yamefikishwa mahakamani ambapo mashauri sita pekee ndiyo yamefikia hatua ya maamuzi na hivyo mashauri 17 kutupiliwa mbali.

Mkwamo huo unaelezwa kudhoofisha juhudi za mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto na wanawake huku jeshi la polisi likitupiwa lawama baada ya mashauri mengi kuhusiana na matukio hayo kushindwa kufikia mafanikio mahakamani.

Kutokana na hatua hiyo, Julai 05, 2019 jeshi la polisi Wilaya Nyamagana linaamua kuwakutanisha pamoja wadau wanaohusika na utoaji haki ikiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Dawati la Jinsia, Ustawi wa Jamii, asasi za kiraia pamoja na watoa huduma za afya ili kujadiliana namna ya kushirikiana kwa pamoja na kuhakikisha kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia zinafikia hatua ya maamuzi mahakamani badala ya kuishia kufutwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Upelelezi (OC-CID) Wilaya Nyamagana, SP. Juma Jumanne akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa Mwanza, Yusto Ruboroga akifungua warsha hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa Mwanza, Betimisimbo Shija akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wadau wa utoaji haki wakifuatilia warsha hiyo.
Lengo la warsha hii ni pamoja na kuweka mikakati ya ushirikiano kwa wadau wote ili kuhakikisha mashauri ya ukatili wa kijinsia yanafikia mafanikio mahakamani.
Wadau wa utoaji haki kama vile Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Dawati la Jinsia, Ustawi wa Jamii, asasi za kiraia pamoja na watoa huduma za afya ili kujadiliana walishiriki kwenye warsha hii.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.