LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCRA yawapiga msasa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imewakutanisha wadau wa mawasiliano kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Sheria inayosimamia biashara ya vifaa vya mawasiliano/ elekroniki na kanuni zake.

Mkutano huo umefanyika jijini Mwanza Novemba 13, 2019 ukiwahusisha maafisa biashara kutoka Halmashauri za mikoa ya Kanda ya Ziwa, makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano, jeshi la pilisi mkoani Mwanza pamoja na viongozi wa umoja wa mafunzi simu Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo alisema ni marufuku kwa wafanyabiashara wote wa vifaa vya mawasiliano/ elekroniki kuagiza, kuuza na kusambaza vifaa hivyo bila kuwa na leseni kutoka TCRA hivyo ni vyema wadau hao hususani maafisa biashara wa Halmashauri wakasaidia utekelezaji wa zuio hilo kwani wanawatambua wafanyabiashara wote katika maeneo yao.

Mhandisi Mihayo alisema hatua hiyo itasaidia kupambana na uuzaji wa vifaa bandia (fake) vya mawasiliano pamoja na wizi wa vifaa hivyo ikiwemo simu ambao hapo awali ulikuwa umeshamiri na na hivyo kusababisha hasara kwa wananchi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye mkutano huo.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakifuatilia mkuatno huo.
Afisa kutoka TCRA Kanda ya Ziwa, William Mnyippembe akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakifuatilia mada kwenye mkutano huo
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia mada.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia mada.
Washiriki wakifuatilia mkutano huo.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.