LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza atangaza Kamati za Maandalizi ya Sherehe za Uhuru 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametangaza Kamati tisa zilizopendekezwa kushiriki kwenye Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika kwa mwaka 2019 zinazotarajiwa kufanyika kitaifa jijini Mwanza.

Mongella ametaja Kamati hizo pamoja na viongozi na wajumbe waliopendekezwa mbele ya kikao cha kwanza cha maandalizi ya sherehe hizo kilichojumuisha pia wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mwanza (KUU) kabla ya mapendekezo hayo kufikishwa katika Kamati ya kitaifa.

Mongella amezitaka Kamati zilizopendekezwa kuwa ni Burudani Habari na Uhamasishaji,  Halaiki, Afya Usafi na Mazingira, Chakula, Fedha na Uwezeshaji, Usafiri Mapokezi na Itifaki, Miundombinu, Sare Mabango na Mapambo pamoja na Usalama.

Kikao hicho cha kwanza cha Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika zinazotarajiwa kuanza Disemba 02, 2019 hadi Disemba 09, 2019 kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Nove,ba 12, 2019.

Itakumbukwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli alitangaza rasmi Sherehe za Uhuru 2019 kufanyika kitaifa jijini Mwanza wakati akizungumza kwenye Baraza la Maulid 2019 lililofanyika kitaifa pia jijini Mwanza, Novemba 10, 2019.
Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Sherehe za Uhuru 2019 kilichofanyika jijini Mwanza.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.