LIVE STREAM ADS

Header Ads

MPC yawashukuru wadau waliofanikisha mkutano wa Marafiki wa Habari Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club- MPC) inatoa shukurani za dhati kwa wadau wote waliofanikisha mkutano wa Wasaa wa Marafiki wa Habari uliofanyika Novemba 09, 2019 ukiwa na lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika kuchochea ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza.
BMG BLOG na BMG TV inakusogezea baadhi ya matukio yaliyojiri kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akifungua mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo ambapo aliahidi ushirikiano wa hali na mali kwa MPC katika kufanikisha ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza.
 Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya wanahabari mkoani Mwanza.
 Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa salamu za ufunguzi kwenye mkutano huo ambapo alisema chama hicho kinaendelea na mikakati yake ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa ofisi na uanzishaji wa redio pamoja na luninga ya mtandaoni.
 Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliahidi milioni 100 kwa MPC ili kuimarisha utendaji wake.
 Mkurugenzi wa taasisi ya Governance Links, Dkt. Donald Kasongi akiwasisha mada kwenye mkutano huo kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika kuchochea maendeleo.
 Mwanahabari, Peter Saramba akiwasilisha mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari.
 Mwakilishi kutoka EWURA akieleza shughuli za taasisi hiyo na mchango wake katika kuchochea maendeleo.
 Mwakilishi kutoka kampuni ya Huduma za Meli Tanzania akielezea miradi inayotekelezwa na kampuni hiyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
 Mwakilishi wa mbunge wa jimbo la Nyamagana akielezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
 Mwakilishi kutoka TCRA akielezea mchango wa taasisi hiyo katika kuchochea maendeleo.
 Mwakilishi kutoka NSSF akielezea mchango wa taasisi hiyo kimaendeleo.
 Mwanahabari Alex Mchomvu akichangia mada kwenye mkutano huo.
 Mwanahabari Moses Methew akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
 Mwanahabari wa siku nyingi, Shija Malando ambaye kwa sasa ni diwani wilayani Kwimba akitoa uzoefu wake kwenye mkutano huo.
 Mmoja wa wanahabari wakongwe mkoani Mwanza akitoa uzoefu wake kwenye tasnia ya habari.
 Mwenyekiti Mstaafu wa MPC, Jimmy Luhende ambaye kwa sasa ni  mkurugenzi wa taasisi ya ADLG akisherehesha mkutano huo.
 Wanahabari na marafiki wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano huo.
 Mkujumbe wa Kamati Tendaji MPC, Nashony Kenedy akitoa neno la shukurani kwenye hitimisho la mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati Tendaji MPC (waliosimama).
 Wanahabari na marafiki wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
Endelea kutazama BMG ONLINE TV hapa chiniNo comments:

Powered by Blogger.