LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella aipongeza REA “wahisani waahidi ushirikiano zaidi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) ameupongeza mpango wa Serikali ya Tanzania wa usambazaji nishati vijijini kupitia REA na kubainisha kwamba ni miongoni mwa mipango bora ya uwezeshaji wananchi kiuchumi barani Afrika.

Mongella alitoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye mkutano wa majumuisho baina ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia mbalimbali wa Maendeleo baada ya kutembelea miradi ya nishati vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa uliofanyika Novemba 22, 2019 jijini Mwanza.

Kando ya mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Julius Kalolo akabainisha kwamba wabia hao wa maendeleo ambao ni pamoja na USAID, SIDA, Benki ya Dunia, Benki ya Afrika pamoja na Nchi za Nordic wameridhishwa na jitihada zinazofanywa na Serikali kusambaza nishati vijijini na hivyo kuahidi ushirikiano zaidi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Julius Kalolo akifafanua jambo kuhusiana na mkutano huo.
 Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Julius Kakolo (wa nne mbele), Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tatu kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tatu kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano huo wa REA na wabia wa maendeleo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.