LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wa dini wasaini makubaliano ya kupambana na Kifua Kikuu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Viongozi wakuu wa dini mbalimbali nchini wamesaini maazimio ya kushirikiana na Serikali, Bunge pamoja na wadau wengine katika kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kupitia nyumba zao za ibada.

Maazimio hayo yalisainiwa Novemba 29, 2019 jijini Mwanza kupitia kikao kilichoratibiwa na wabunge wanaoshiriki kwenye mapambano dhidhi ya TB chini ya ulezi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pindo ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya Agri-Thamani huku mgeni rasmi akiwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Spika wa Bunge wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akizungumza kwenye kikao hicho cha viongozi wakuu wa dini kusaini maazimio ya kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.
 Waziri Mkuu Mstaafu Serikali ya awamu ya nne, Mizengo Pindo ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya Agri-Thamani akitoa salamu zake kwenye kikao hicho.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa salamu zake kwenye kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake.
 Mwakilishi wa viongozi wakuu wa dini Tanzania, Jacob Chimeledya ambaye pia ni Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) akisoma maazimio ya viongozi hao kushiriki kwenye mapambano dhidi ya Kifua Kikuu.
 Viongozi wakuu wa dini Tanzania kwa pamoja wamekubaliana nyumba zao za ibada kutumika kwa ajili ya kufikisha elimu ya kujikinga na Kifua Kikuu.
 Viongozi wakuu wa dini mbalimbali Tanzania wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa afua mbalimbali za kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu.
 Taswira mwonekano wa kikao hicho.
 Kikao hicho kilifanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
 Viongozi wakuu wa dini mbalimbali nchini wakisaini maazimio ya kushiriki kwenye mapambano dhidi ya Kifua Kikuu.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.