LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yahitimishwa jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Disemba 01, 2019 Tanzania imeungana na mataifa mengine kuadhimisha kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani ambapo kitaifa yalifanyika viunga vya Rock City jijini Mwanza.

Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama aliyemwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi wakati akiwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Colonel Magembe.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa salamu za Wizara kwenye kilele cha maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu za Mkoa kwenye maadhimisho hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akitoa pongezi kwa viongozi mkoani Mwanza kwa kusaidia maadhimisho hayo kufana.
 Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Leticia Kapela akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo.
 Wanaharakati kutoka mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo KIVULINI wakiingia kwenye maadhimisho hayo huku wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali.
 Jumbe mbalimbali kutoka kwa wadau walioshiriki maadhimisho hayo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.