LIVE STREAM ADS

Header Ads

Asilimia tano ya almasi ya Mwadui kuuzwa Maganzo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Mdini, Doto Biteko amemwagiza Afisa Madini Mkoa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu kuhakikisha hadi ifikapo Disemba 22, 2019 awe ameandaa utaratibu mzuri wa kutoa mchanga wa madini ya almasi (makinikia) nje ya mgodi wa Mwadui (Williamson Diamond Limited) na kuwapatia wachimbaji wadogo.

Aidha Biteko amesisitiza kwamba kuanzia mwezi Januari 2020 uongozi wa mgodi huo uzingatie maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya kuhakikisha asilimia tano ya almasi inayozalishwa mgodini hapo inaanza kuuzwa kwenye masoko ya ndani ikiwemo Maganzo badala ya mzigo wote kusafirishwa kwenda Ulaya.

Biteko aliyasema hayo Disemba 10, 2019 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo katika Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga baada ya kufanya ziara katika mgodi wa Mwadui na kisha kuzungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi ambapo aliwapongeza kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji na hivyo kutoa maelekezo kwa uongozi kuzingatia maslahi yao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Mdini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya almasi katika eneo la Magazo, Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga.
 Baadhi ya wachimbaji wadogo wa almasi wakimsikiliza Waziri wa Mdini, Doto Biteko.
 Baadhi ya wachimbaji wa almasi wakifuatilia mkutano huo ambapo walipokea kwa furaha maelekezo ya kupewa mchanga wa almasi (makinikia) ambayo wamekuwa wakiyaomba kwa muda mrefu.
 Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack akitoa salamu zake kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mdini, Doto Biteko ili kuzungumza na wachimbaji wadogo wa almasi katika eneo la Maganzo.
 Mkuu wa Wilaya Kishapu, Nyabaganga Talaba alisema mazungumzo na uongozi wa mgodi wa Mwadui yanaendelea ili kufikia mwafaka wa mgodi kutoa ushuru wa asilimia 0.7 kuchangia huduma za kijamii (CSR) pamoja na asilimia 0.3 kama ushuru wa huduma (Service Levy).
 Mbunge wa Kishapu, Selemani Nchambi alisema mchanga wa madini uliotolewa ajili ya wachimbaji wadogo kupitia vikundi vyao utawanufaisha kiuchumi.
 Awali Waziri wa Mdini, Doto Biteko akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Mwadui.
 Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa almasi wa Mwadui wakimsikiliza Waziri wa Mdini, Doto Biteko.
 Mmoja wa wafanyakazi wa mgodi wa Mwadui, Zaituni Jafari akiuliza jambo kwenye mkutano huo.
 Meneja Mkuu wa mgodi wa Mwadui akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Waziri wa Mdini, Doto Biteko (kushoto) akikagua kitabu cha mauzo kwa mmoja wa wanunuaji na wauzaji wa madini alipotembelea soko la madini Maganzo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.