LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko akabidhi leseni 10 kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko amekabidhi leseni kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Wilaya Nzega mkoani Tabora na kutumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria.

Biteko amekabidhi leseni hizo Disemba 07, 2019 baada ya Serikali kuridhia kuwapatia wachimbaji wadogo sehemu ya eneo lililokuwa mgodi wa Resolute ambao shughuli za uchimbaji ulifikia ukomo ambapo kwa sasa linamilikiwa na Chuo Cha Madini Dodoma.

Vikundi vilivyokabidhiwa leseni ni Msilale Miners Group, Jimbo la Nzega Vijijini, Undomo Miners Group, Hapa Kwetu Group, Umoja wa Wachimbaji Mwanshina, Mkombozi Mining Group, Imalamakoye Miners Group, Salama Miners, Makalanga Minerals Group na Nzega Miners Association.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko akikabidhi leseni kwa mmoja wa wawakilishi wa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Wilaya Nzega mkoani Tabora. 
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Zega kabla ya kukabidhi leseni za uchimbaji dhahabu kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya Nzega mkoani Tabora, Godfrey Ngupula akiahidi kusimamia vyema shughuli za uchimbaji dhahabu wilayani humo ili kuleta tija kwa wachimbaji wadogo.
 Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Tabora, Baraka Mbasa akitoa shukurani kwa Serikali kupitia Waziri wa Madini baada ya kuridhia kuwakabidhi wachimbaji wadogo leseni za uchimbaji dhahabu.
 Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Nuru Shaban ameahidi kutoa nafasi ya masoko kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Nzega ili wajifunze namna bora na salama ya kufanya shughuli zao.
 Katibu wa Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe akitoa shukurani baada ya Serikali kuwakabidhi wachimbaji wadogo wa dhahabu jimboni humo leseni ya uchimbaji.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko alifika katika shimo namba tano la uliokuwa mgodi wa Resolute na kutoa angalizo kwa kikundi kitakachokuwa kinafanya shughuli za uchimbaji jirani na eneo hilo kuandaa mkakati wa kiusalama kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji.
 Shimo namba tano la uliokuwa mgodi wa Resolute ambao shughuli za uchimbaji ulifika ukomo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.