Biteko afungua soko la madini Chato "atoa wiki moja kwa RMO Geita"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa
Madini, Doto Biteko Disemba 27, 2019 amefungua rasmi soko kuu la madini Wilaya Chato eneo la Buseresere mkoani Geita na kutumia fursa hiyo kuwataka maafisa wa Serikali kutowabugudhi wanaokwenda kuuza
madini yao kwenye masoko yanayoanzishwa kote nchini kwa kigezo cha kutaka kujua
walikoyatoa.
Aidha Biteko
ametoa muda wa wiki moja kwa Afisa Madini Mkazi Mkoa Geita (RMO), Mhandisi Daniel
Mapunda kuhakikisha anatoa leseni kwa wale wote wenye mitambo ya kuchenjulia
madini akisema mkoani Geita kuna jumla ya mitambo 278 ambayo bado haijapata
leseni hatua ambayo inaikosesha Serikali mapato.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: