LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tuzo za Cheza Kidansi 2019 zatolewa jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.comJudith Ferdinand,Mwanza
Na Judith Ferdinand, MwanzaTuzo za Cheza Kidansi 2019 nchini Tanzania zimetolewa Disemba 21, 2019 jijini Mwanza huku wanamuziki 12 wakiibuka kidedea akiwemo Diamond Platnumz aliyeibuka mshindi kipengere cha msanii mwenye mchango mkubwa kwenye muziki wa dansi.

Washindi kwa msimu huu wa kwanza walioibuka kidedea ni rapa bora Totoo Kalala, mpigaji bora wa chombo Dekanto Bass, mwanamuziki chipukizi Kelly Haso, mtayarishaji bora Erasto Mashine, mnenguaji bora Queen Suzy, mtunzi bora Jimy Manzoka, video bora chozi langu ya Jimy Manzoka.

Nafasi ya mwanamuziki bora Nyoshi El Saadat, wimbo bora ukiwa usiku wa manane kutoka Mjengoni Classic Band, bendi bora Sky Melodies, tuzo ya heshima akitunukiwa King Kikii.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo hizo zilizotolewa jana Jijini Mwanza, Agnes Kiwanga kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) aliwataka wasanii wa dansi kutokata tamaa kutokana na changamoto wanazozipitia bali wazitumie kuwa fursa itakayowapatia matunda na chamsingi ni kufanya kazi zilizo bora za kisanaa zenye maadili kwa mwimbaji na mtazamaji ili waweze kupata tuzo za kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake Mratibu wa tunzo hizo, Bernard James alisema wamejipanga kuchochea mziki wa dansi kutoka hapo ulipo kwenda hatua nyingine hivyo ushirikiano ukiwepo watalifanikisha hilo kwa kuwa wameanza na ushindi wa kufanikisha vyema warsha hiyo,wametambua, wamethamini na wanaunga mkono jitihada, juhudi na maarifa katika mziki wa dansi ili kuhakikisha unasonga mbele lakini ushirikiano unahitajika katika kutekeleza adhima hiyo.

"Mashindano haya tulianzisha mwaka huu yenye lengo la kuinua na kuuthamini mziki wa dansi nchini uliokuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi hivyo uanzishwaji wa tuzo itakuwa chachu ya kuleta ushindani na mafanikio katika sekta hii" alisema James.

Pia aliwataka wasanii kujitokeza kwa wingi kumenyana kwenye mashindano hayo ambayo yatakuwa endelevu hivyo waongeze ubunifu na kufanya utafiti kujua washabiki wao wanataka nini ili kutoa kitu kilicho na ubora na kuchochea mziki kwenda mbele zaidi.

Rapa bora Totoo Kalala na mwanamuziki chipukizi Kelly Haso walisema ushindi huo umewaongezea chachu kwenye safari yao ya muziki wakisema tuzo za muziki wa dansi Tanzania zitaongeza ushindaji katika kazi zao.

No comments:

Powered by Blogger.