LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waandishi wa Habari wakumbushwa kujiendeleza kitaaluma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliolenga kujadili Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na utangazaji ukiandaliwa na Klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuasisiwa kwake Disemba 09, 1994.

Mkutano huo umefanyika Disemba 04, 2019 jijini Mwanza ukihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo Soko amesema Klabu hiyo inafanya juhudi mbalimbali ili kuhakikisha wanachama wake wanajiendeleza kitaaluma, kuzifahamu Sheria za Habari na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amewapongeza waandishi wa habari ambao tayari wameanza kujiendeleza kielimu ili kuendana na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 inayotaka mtu anayefanya kazi ya uandishi wa habari na utangazaji kuwa na elimu kuanzia ngazi ya Stashahada ya taaluma hiyo.

"Pia nawapongeza wamiliki wa vyombo vya habari ambao wameanza kuzingatia matakwa ya sheria ili kulinda tasnia ya vyombo vya habari, hakika kufanya hivyo ni kuijenga, kuijali na kuiheshimu tasnia yenu ya habari" ameongeza Mhandisi Kilaba akisisitiza waandishi wa habari wasio na sifa kitaaluma kujiendeleza kabla ya nwaka 2022.

Hata hivyo baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa na mtizamo tofauti kuhusiana na sifa hiyo ya elimu katika taaluma ya habari wakisema inaminya uhuru wa habari na kwamba mwenye taaluma ya habari kuanzia ngazi ya cheti angeendelea kutambulika kama ilivyo katika kada nyingine za kitaaluma.
#BMGHabari
 Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsani amesema ni vyema waandishi wa habari wakajiendeleza kielimu ili kutokinzana na sheria huku akitoa rai kwa MPC kuandaa vitambulisho (Press Card) pamoja na vikoti maalum vya habari (Press Jackets) na kuvigawa kwa wanachama wake ili kurahisisha utendaji kazi wao hususanyi wakati wa chaguzi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, Mhandisi James Kilaba (katikati) pamoja na Meneja wa Kanda wa mamlaka hiyo, Mhandisi Francis Mihayo (kushoto) wakiwa kwenye mkutano hu. Kulia ni Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko.
 Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakiwa kwenye mkutano huo.
 Waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya habari wakifuatilia mkutano huo.
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano huo. 

No comments:

Powered by Blogger.