LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wazee wa mila wakubali kushiriki mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wazee wa mila kutoka mikoa tisa nchini yenye kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia wamekubaliana kutumia ushawishi walio nao ili kwenye mapambano dhidi ya vitendo hivyo ikiwemo ukeketaji, kutakasa wanawake, mimba na ndoa za utotoni.

Wazee hao wamefikia maazimio hayo Disemba 05, 2019 jijini Mwanza kwenye mkutano ulioshirikisha viongozi wa mila zaidi ya 200 kutoka makabila mbalimbali ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi na Manyara ulioandaliwa na shirika la UN Women.

Hata hivyo mmoja wa wazee hao, Chifu Mfungo Charles kutoka mkoani Geita amesema changamoto waliyonayo ni kukosa nguvu kisheria na hivyo kuomba Serikali kuwarejeshea mamlaka waliyokuwa nayo hatua itawaongezea nguvu ya kupambana na yeyote atayekumbatia mila zinazochochea ukatili wa kijinsia.

Kwa upande Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha amesema wazee wa mila ni wadau muhimu katika kutokomeza mila na desturi zinazorudisha nyuma maendeleo ya wanawake hivyo kuwashirikisha kwenye mapambano hayo kutasaidia kuleta mabadiliko katika jamii zao ikiwemo kuwashirikisha wanawake katika shughuli za kiuchumi.

Itakumbukwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha ukatili nchini ni Mara asilimia 78, Shinyanga asilimia 78, Tabora asilimia 71, Kagera asilimia 67, Geita asilimia 63, Simiyu asilimia 62, Kigoma asilimia 61, Mwanza asilimia 60, Njombe asilimia 53, Dodoma asilimia 50 na Katavi asilimia 50.
Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha akiwahimiza wazee wa mila kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi na Manyara kutumia ushawishi wao katika jamii kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
 Wazee wa mila kutoka mikoa tisa nchini yenye kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia wakifuatilia mkutano huo.
Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha akifafanua jambo kwa wazee wa mila waliohudhuria mkutano huo.
 Wazee wa Mila kutoka mikoa tisa nchini yenye kiwango kikubwa cha vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa kwenye mkutano wa kujengeana uwezo na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo hivyo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.