LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wazee wa mila wajengewa uwezo kushiriki mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kiuchumi (UN Women) limewakutamisha wazee wa mila kutoka mikoa tisa nchini yenye changamoto ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuwajengea uwezo na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo hivyo.

Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha amesema wazee hao wakipata elimu watasaidia kuleta mabadiliko katika jamii zao ikiwemo kupambana na ukatili wa kijinsia, kuchochea usawa wa kijinsia, kusomesha watoto wa kike na wanawake kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI, Yassin Ally amesema wazee wa mila wamekuwa wakitoa adhabu mbalimbali za kimila kwa wanajamii wanaokiuka desturi zao hivyo baada ya kujengewa uwezo watakuwa na wajibu wa kueleza wazi ni adhabu gani zinaweza kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba na ndoa za utotoni katika maeneo yao huku wakienzi na kuendeleza mila nzuri.

Baadhi ya wazee wa mila washukuru kushirikishwa kwenye kikao hicho na kuahidi kufikisha elimu waliyoipata kwa wenzao ili kuhakikisha wanatokomeza mila na desturi zinazochochea ukatili wa kijinsia katika jamii.

Kikao hicho cha siku mbili kuanzia Disemba 04, 2019 jijini Mwanza kimejumuisha wazee wa mila zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi pamoja na Manyara.
Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha akitoa neno la ufunguzi wa kikao hicho na malengo yake ambayo ni pamoja na kuwajumuisha wazee wa mila katika kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye kikao hicho kilicholenga kuwajengea uwezo wazee wa mila kutoka mikoa tisa ya Tanzania yenye kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akichangia mada.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Baadhi ya wazee wa mila walioshiriki kikao hicho wakifuatilia mada kwa umakini.
Wazee wa mila kutoka mikoa tisa ya Tanzania wakifuatilia kikao hicho.
Wazee wa mila wanajengewa uwezo ili kuwa wana mabadiliko katika kuleta usawa wa kijinsia kwenye maeneo yao huku wanawake wakipata fursa ya kushiriki kwenye nyanja za maendeleo.
Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wazee wa mila kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi na Manyara wakifuatilia kikao hicho.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimelenga kuhamasisha wazee wa mila kushiriki kwenye juhudi za kuleta usawa wa kijinsia katika jamii na kupiga vita aina zote za vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Washiriki wa kikao hicho wameaswa kutokumbatia mila na desturi zinazochochea ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike.
Wazee wa mila kutoka mikoa tisa ya Tanzania walioshiriki kikao wakinyoosha mikono juu kaka ishara ya kuunga mkono hoja kwenye kikao hicho.
Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha (kulia) akifurahia wimbo wa asili na wazee wa milaa walioshiriki kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakicheza wimbo wa kisukuma.
Wazee wa mila walioshiriki kikao hicho wakifurahia burudani ya asili kutoka kabila la wasukuma.
Baadhi ya wazee wa kimila kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi na Manyara walioshiriki kwenye kikao hicho.
Takwimu inayoonyesha mikoa yenye changamoto ya ukatili wa kijinsia Tanzania.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.