LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tume yaundwa kuwabaini wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Magu mkoani Mwanza, Dkt. Philemon Sengati amebainisha kuundwa kwa tume ndogo kwa ajili ya kubaini baadhi ya watumishi katika taasisi mbalimbali ikiwemo za elimu wilayani humo ambao wanajihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

Dkt. Sengati aliyasema hayo Disemba 03, 2019 wakati akifungua kikao cha viongozi na watendaji mbalimbali wilayani humo wakiwemo maafisa maendeleo ya jamii, elimu, afya, mahakama pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama kwa lengo la kuweka mikakati ya kupambana na mimba/ ndoa kwa wanafunzi.

Aidha alibainisha kwamba changamoto ya mimba kwa wanafunzi wa kike wilayani humo ni kubwa ambapo kwa mwaka huu tayari wanafunzi 34 wa Shule za Msingi pamoja na 65 wa Shule za Sekondari wameripotiwa kupewa mimba.

Naye Yassin Ally ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI linaloshirikiana na Halmashauri ya Wilaya Magu kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia alitoa rai kwa mamlaka za utoaji haki ikiwemo polisi na mahakama kuepuka umalizaji wa mashtaka ya ukatili wa kijinsia kama vile ubakaji kwa madai ya kukosa ushahidi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao hicho.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba akisisitiza viongozi wote kuungana ili kupambana na mimba kwa wanafunzi.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba amesema mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Magu, Hilal Elisha akisisitiza ushirikiano zaidi ili kufanikisha mkakati wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni katika Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally ametaka elimu kuendelea kutolewa kwa jamii ili kutoa ushahidi mahakamani kwani mashtaka mengu ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakifutwa kwa kukosa ushahidi.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally pia ametoa rai kwa mamlaka za utoaji haki kuendelea kutimiza vyema wajibu wake ikiwemo kuwatia hatiani wanaobainika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally pia ametoa rai kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kama vile kubakwa kuwahi katika vituo vya afya ndani masaa 72 ili kupata huduma ya matibabu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Magu, Edmond Kente baadhi ya mashtaka ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakikosa mafanikio mahakamani kutokana na wananchi kutokuwa tayari kutoa ushahidi.
Mkuu wa Polisi Wilaya Magu, SSP. Mahamoud Banga ametoa rai kwa wananchi kuwa tayari kutoa ushahidi wanapohitajika katika kesi za ukatili wa kijinsia ili kurahisha uharaka wa upelelezi wa kesi za aina hiyo.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Magu, Susan Mwendi akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Magu, Coretha Sanga akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mganga Mkuu Wilaya Magu, Dkt. Maduhu Nindwa akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Katibu wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya Magu, Sauda Kenganya amesisitiza malezi bora kwa watoto hatua itakayosaidia kuwakinga na vitendo viovu ikiwemo mimba katika umri mdogo.
Viongozi mbalimbali wilayani Magu wakifuatilia kikao hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Watendaji mbalimbali wilayani Magu wakifuatilia kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakinasa mikakati iliyokuwa ikijadiliwa.
Watendaji na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.