LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wakabidhi vitendea kazi wilayani Misungwi baada ya mradi kufikia ukomo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Shirika la Global Affair la nchini Canada limekabidhi vitendea kazi vya aina mbalimbali ikiwemo pikipiki, kompyuta mpakato pamoja na fanicha za ofisini katika Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kuhitimisha utekelezaji wa mradi wa Mama na Mtoto katika Halmashauri hiyo.

Utekelezaji wa mradi huo ulianza mwaka 2016 na umefikia tamati mwaka huu 2019 ambapo ulikuwa na lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kusaidia uboreshaji huduma za afya ikiwemo ujenzi wa majengo ya kutolea huduma, vifaa tiba pamoja na kuwajengea uwezo/ elimu watoa huduma za afya wilayani Misungwi ili kuendeleza huduma bora hata mradi ukifikia ukomo.
#BMGHabari
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Kisena Mabuba (kulia) akipokea vitendea kazi mbalimbali ikiwemo pikipiki, kompyuta mpakato pamoja na fanicha za ofisini baada ya mradi wa Mama na Mtoto uliokuwa unatekelezwa na Shirika la Global Affair la nchini Canada kufikia tamati. Katikati ni Mwakilishi wa Shirika hilo, Sanya Salewiski.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.