LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanachama wa TAHA watembelea mashamba kujifunza Kilimo chenye Tija

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wanachama wa taasisi ya kilimo cha mboga mboga na matunda TAHA (Tanzania Horticultural Association) mkoani Mwanza, wametembelea mashamba mbalimbali ya wakulima wenzao wanaopata elimu na mafunzo kuhusu namna bora ya kuendesha kilimo chenye tija ili nao kujifunza namna ya shughuli zao.

Wanachama hao ambao pia ni wakulima wa mboga na matunda walitembelea mashamba hayo Disemba 16-17, 2019 katika Wilaya za Mkoa Mwanza ikiwemo Magu na Nyamagana na kujifunza kwa vitendo mbinu bora za kilimo cha mazao kadhaa ikiwemo papai.

Taasisi ya TAHA bado inaendelea kutoa nafasi kwa wakulima kujiunga na taasisi hiyo kupitia vikundi vyao kwa ada ya shilingi elfu ishiriki (Tsh. 20,000) kwa mwaka ama shilingi laki moja (Tsh. 100,000) kwa mwaka ikiwa ni mwanachama mmoja mmoja na kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo pamoja na masoko.

Pichani juu ni wanachama hao wakiwasili katika shamba mapapai katika Kijiji cha Bundilya wilayani Magu ambalo linamilikiwa na mmoja wa wakulima ambaye pia ni mwanachama wa TAHA.
Wakulima wa mbogamboga na matunda ambao pia ni wanachama wa TAHA wakijifunza kilimo bora cha zao la nyanya katika shamba darasa la taasisi hiyo lililopo katika eneo la Nanenane wilayani Nyamagana.
Wakulima wa mbogamboga na matunda ambao pia ni wanachama wa TAHA wakijifunza namna ya kuendesha kilimo cha papai katika shamba la mmoja wa wanachama wa taasisi hiyo katika Kijiji cha Bundilya wilayani Magu.
Wakulima ambao pia ni wanachama wa TAHA wakijifunza namna bora ya kuendesha kilimo cha zao la nyanya katika shamba darasa la TAHA eneo Nanenane wilayani Nyamagana.
Mkuu wa wilaya ya Magu, Dkt. Philemon Sengati akizungumza na wakulima katika Kijiji cha Bundilya wilayani humo na kuwahimiza kutumia vyema mafunzo wanayoyapa kupitia taasisi ya TAHA ili kuboresha shughuli zao na kujiongezea kipato.
Wanachama wa Taasisi ya TAHA mkoani Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati na viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini
Picha na Michael Jamson, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.