LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ujenzi jengo la abiria MWANZA AIRPORT wapata Baraka za Waziri Mkuu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Disemba 08, 2019. Ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Septemba 25, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Magufuli alilolitoa Julai 15, 2019 wakati akizindua miradi ya afya katika Hospitali ya Bugando. 

Muda wa ujenzi huo ulipangwa kuwa miezi 12 lakini kasi ya ujenzi wake inafanyika usiku na mchana ili likamilike ndani ya miezi sita ambapo linajengwa kupitia mfumo wa "Force Account" chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza huku likitarajiwa kugharimu bilioni 12 (Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela zikichangia Bilioni nne) hadi kukamilika.
 Msimamizi Mkuu wa ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi Tunaye Mahenge (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa kwanza kushoto) kuhusiana na mradi huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Ujenzi wa jengo la abiria Mwanza Airport baada ya miezi miwili

No comments:

Powered by Blogger.