LIVE STREAM ADS

Header Ads

Balozi wa Namibia afanya ziara Mwanza “abaini fursa kiuchumi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Theresia Samaria (kushoto) amefanya ziara ya kutembelea viwanda mbalimbali vya kuchakata minofu ya samaki jijini Mwanza na kubaini uwepo wa fursa za kiuchumi baina ya wafanyabiashara wa nchi zote mbili.

Samaria amefanya ziara hiyo Januari 20, 2020 akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) na kutembelea kiwanda cha OMEGA Fish Ltd, Nile Pitch pamoja na soko la mazao ya samaki Mwaloni Kirumba. Pia alitembelea kilichokuwa kiwanda cha ngozi cha Mwanza Tanneries ambacho juhudi za kukifufua zinaendelea kufanywa na Serikali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kiwanda cha kuchakata samaki Nile Pitch jijini Mwanza.
 Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Theresia Samaria alipotembelea soko la kimataifa la mazao ya samaki Mwaloni Kirumba jijini Mwanza.
 Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Theresia Samaria akiwa katika eneo la soko la Mwaloni Kirumba.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Theresia Samaria (kulia) akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiangalia baadhi ya mitambo katika kiwanda cha ngozi Mwanza Tanneries.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.